Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:44 pm

NEWS: UJURUMANI KUTOA MILIONI 9 KWA KILA MUHAMIAJI ATAKAYE REJEA KWAO

Berlin: Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere ameliambia gazeti la Bild am Sonntag kuwa wahamiaji wote ambao maombi yao ya kupata hifadhi yamekataliwa kuondoka nchini humo kwa hiari na kurejea kwenye nchi wanazotoka na pia wanaweza kupewa msaada wa kifedha wa Euro 3,000 sawa na Tsh milioni 8.6 kila mmoja .

De Maiziere amesema kwamba mpango huo ni kwa ajili ya kuwasaidia kutengamana tena pindi watakaporejea nchini mwao. Kwa miaka kadhaa Ujerumani imekuwa ikitoa msaada wa fedha kwa wahamiaji wote waliokataliwa kupewa hifadhi, ili kuwasaidia waweze kurejea kwenye nchi zao, zikiwemo gharama zinazohusiana na safari pamoja na fedha za kuanzia maisha pindi watakaporejea.

"familia zinaweza kupatiwa hadi Euro 3,000 na mtu mmoja mmoja akipatiwa hadi Euro 1,000 kama wataamua kurejea nyumbani kwa hiari ifikapo mwishoni mwa mwezi Februari. ''Ukiamua kurejea nyumbani kwa hiari ifikapo wakati huo, ili kukusaidia kuanza maisha mapya, unaweza ukapewa fedha za kugharamia makaazi kwa mwaka mmoja ukiwa kwenye nchi yako,'' amesema de Maiziere.