- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : UINGEREZA INA SHAUKU YA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA NA IRAN
Uingereza ina hamu ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameashiria namna Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilivyoheshimu vizuri makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa London ina hamu ya kuona uhusiano wake wa kibiashara na Tehran unaimarika.
Shirika la habari la IRNA limemnukuu Boris Johnson akisema hayo jana (Jumatano) mbele ya bunge la Uingereza na kusema kuwa, serikali ya nchi yake haipendi kuona Marekani inarejesha vikwazo vyake dhidi ya Iran kwani vitayaathiri mashirika ya Uingereza.
Amesema, mashirika ya Uingereza yana hamu ya kuwa na ushirikiano mzuri wa kibiashara na Iran na kuongeza kuwa, London haipendi kuona hatua mpya za Marekani zinathiri makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kufikia hatua ambayo Iran itayaona makubaliano hayo hayana faida tena.
Makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1 linaloundwa na Uingereza, Ufaransa, Russia, China, Marekani na Ujerumani yalianza kutekelezwa mwezi Januari 2016, lakini Marekani licha ya kuwa ni mmoja tu kati ya waliotia saini makubaliano hayo yenye baraka kamili za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inadharau haki za pande zote hizo na kufanya njama za kila namna za kukwamisha utekelezaji wa makubaliano hayo.
Tarehe 13 mwezi huu wa Oktoba, Rais wa Marekani, Donald Trump alidharau ripoti nane za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA zilizothibitisha kwamba Iran imeheshimu kukamilifu makubaliano ya JCPOA na badala yake alisema, hawezi kuunga mkono taarifa kuwa Iran imeheshimu makubaliano hayo, bali hata alitishia kujitoa kwenye JCPOA.