Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:00 pm

NEWS: UFARANSA KUYAONGEZEA KODI MAKAMPUNI YA "GOOGLE, FACEBOOK, TWITTER

Ufaransa imesema kuwa itaongeza kodi yake kwenye kampuni kubwa za intaneti na teknolojia kama Google , Facebook, Twitter, Whatsup, Apple, Amazon N.k kuanzia mwezi Januari, ikiwa Umoja wa Ulaya utashindwa kukamilisha utaratibu wa kulipa kodi mpya ya kikanda.

Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire amesema leo kuwa kodi hiyo itaanzishwa kwa vyovyote vile Januari Mosi, na itatozwa kwa mwaka wote wa 2019 kwa kiwango kinachokadiriwa kufikia euro milioni 500.

Ufaransa imekuwa ikishinikiza kuanzisha kodi mpya inayojulikana kama GAFA, jina linalotokana na makumpuni ya Google, Apple, Facebook na Amazon, kuhakikisha kuwa mashirika hayo makubwa duniani yanalipa kodi ya haki kutokana na operesheni zao za kibishara barani Ulaya.

Kiwango kidogo cha kodi kinacholipwa na mashirika hayo ya Kimarekani kimekuwa kikizusha hasira mingoni mwa wapigakura katika mataifa mengi ya Ulaya, lakini kanda hiyo yenye wanachama 28 imegawika juu ya namna ya kushughulikia suala hilo.