- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UDART YATOA UFAFANUZI KUUNGUA KWA BASI LA MWENDOKASI
Dar es salaam: Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (UDA-RT) imetoa ufafnuzi juu ya chanzo cha ajali iliyotokea mchana wa mwezi Desemba 25, mwaka huu eneo la Ubungo Maji kwamba ajali hiyo ilitokana na hitilafu ya mfumo wa umeme katika Basi hilo.
Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, John Nguya kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 155 ,lilikuwa likitokea Kimara kwenda Gerezani lilishika moto kwenye injini na kuwatia hofu abiria na wananchi wengine.
Alisema kuwa moto huo ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa wananchi waliokuwa eneo hilo,Jeshi la Zima Moto na Uokoaji , Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa UDART kwa kutumia vifaa vya kuzima moto vilivyomo kwenye magari hayo.
“Tungependa wananchi wafahamu kwamba usalama wa mabasi yote ya UDA -RT umedhibitiwa kwa asilimia 100 kuwa matengenezo take yanafanyika kwa umahiri ,viwango vya kimataifa kwa wasimamizi na watalaam kutoka kampuni ya Xiamen Golden Dragon ya China, Cummings ya Marekani ya kimataifa na Voith ya Ujerumani.
“Ndani ya mabasi hayo eneo la injini vipo vizimia koto vitatu vilivyotengenezwa humor na kuzima moto baada ya koto kuzidi na ndivyo ilivyokuwa wakati wa tukio na pia mabasi makubea kuna vizimia moto vinne vyenye ujazo wa kilogramu tatu katika kila mlango mikubwa ya pande zote mbili kwa akili ya dharura,” alisema Nguya.