- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UCHAGUZI NCHINI CONGO WAHAIRISHWA KWA WIKI MOJA
Tume ya uchaguzi nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) imetangaza kuahirisha kwa wiki moja uchaguzi mkuu uliokuwa umepangiwa kufanyika Jumapili hii.
Uchaguzi huo sasa umepangiwa kufanyika Jumapili tarehe 30 Desemba badala ya tarehe 23 Desemba.
Tume hiyo imesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuchelewa kwa shughuli ya kufikisha vifaa na mitambo ya kupigia kura vituoni.
"Tumewaambia mafundi wetu ya kwamba wafanye juhudi zao zote ili uchaguzi ufanyike Disemba 23, lakini kila wakati tunaangalia wapi walipofika. Kama haiwezekani tunapanga kuongea na wanasiasa ili kuangalia namna gani tutaweza kuahirisha uchaguzi na kuongeza siku nne, saba au 14 na sioni wapi kuna ubaya wakati tunataka kufanya mambo kwenye utaratibu mzuri," alisema Kalamba Alhamisi.
Tangazo hilo la ghafla linatokea wakati polisi walimzuia mmojwapo wa wagombea wakuu wa upinzani wa kiti cha urais Martin Fayulu kuzindua kampeni zake katika mji mkuu wa nchi hiyo.