- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UCHAGUZI KENYA KIZUNGUMKUTI, TUME (IEBC) YAGAWANYIKA
Nairobi: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati amesema hawezi kujiuzul baada ya mmoja wa Makamishena wa Tume hiyo Roselyn Akombe kutangaza kujiuzulu mapema jana 17.8.2017.
Chebukati amekiri kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya Tume hiyo na maelekezo yake kama ya kisheria wakili na Mwenyekiti, yamekuwa hayaungwi mkono na Makamishena wote ndani ya Tume hiyo.
“Sina uhakika iwapo Uchaguzi utakuwa huru na haki, na iwapo nitakuwa Mwenyekiti wa Tume hii katika mazingira haya,” amesema.
"Nawaomba Watumishi ndani ya Tume ya Uchaguzi waliotajwa wajiuzulu, sitaki jina langu kuharibiwa katika Uchaguzi huu,".
Chebukati amesema anajitahidi kadri awezavyo kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa tarehe 26 unafanyika, ingawa kunamazingira magumu lakini inavyoonekana ni ngumu.
Aidha, amesema anawapa kadi ya njano wanasiasa nchini humo na kuwataka kuacha kuwatisha Makamishena na wafanyikazi wa Tume hiyo, ili watekeleze majukumu yao ipasavyo.
“Nilipewa kazi hii, kuhakikisha kuwa naitumikia nchi yangu na kuhakikisha kuwa Uchaguzi unafanikiwa na hili nitahakikisha kuwa linafanyika,” alisema Chebukati.
“Kujiuzulu lingekuwa jambo rahisi sana kufanya hivyo kwangu hasa kipindi hiki lakini sitajiuzulu,” aliongeza.
Mgawanyiko ndani ya Tume ya Uchaguzi, umezua wasiwasi iwapo usimamizi huo utakuwa huru na haki.
Rais Uhuru Kenyatta mapema siku ya Jumatano, alitangaza kuwepo kwa maombi ya kitaifa nchini humo na kusisitiza kuwa ni lazima Uchaguzi huo unafanyika wiki ijayo.
Hata hivyo, kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, amesema hatashiriki katika Uchaguzi huo iwapo mabadiliko hayatafanyika.