- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TUME YA UCHAGUZI CONGO YAHAIRISHA KUTANGAZA MATOKEO
Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hatimaye imeahirisha kutangaza matokeo ya awali ya Uchaguzi wa urais, baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka 2018 mpaka wiki Ijayo.
Raia wa DRC walikuwa wamesubiri kutolewa kwa matokeo hayo, hivi leo kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetangazwa hapo awali na Tume ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Corneille Nangaa amesema siku ya Jumapili, haitawezekana kutangaza matokeo hayo kwa sababu mchakato huo bado haujapatikana.
Tume ya Uchaguzi haijatangaza tarehe ya kutolewa kwa matokeo hayo wakati huu, wananchi wakisubiri matokeo hayo kwa hamu licha ya kuwepo kwa hali ya wasiwasi.
Ushindani mkali unashuhudiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi wote kutoka upande wa upinzani.