- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRUMP NA RAIS WA IRAN WARUSHINA MANENO MAKALI
New York: Leo Jumatano umeendelea kufanyika mkutano wa 73 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo Rais wa Marekani Donald Trump na Mwenzie wa Iran Hassan Rohan kutunishiana misuli baina yao, wote wakituhumiana vikali kuhusiana maswala mbali mbali.
Kila mmoja katika mkutano huo alipewa nafasi ya kuzungumza.
Miezi michache baada ya Marekani kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia, Rais wa Marekani amezitaka nchi nyingine kuchukua hatua kama hiyo: "Serikali ambayo kauli yake mbiu ni" Kuiona Marekani imeangamia"na kuitishia Israeli kwamba itageuzwa jivu mara moja, haiwezi kuwa na nia njema ya kusitisha mpango wake wa nyuklia. Haiwezekani. Tunatoa wito kwanchi zote ulimwenguni kutenga utawala wa Iran wakati ambapo itakuwa bado na mpango wake wa kuendeleza ukandamizaji wake. "
Kwa upande wake, Rais wa Iran, Hassan Rohani amesema hashangazwi na msimamo wa Donald Trump, ambaye amezitaka nchi zote duniani kuitenga Iran. Hassan Rohani ameishtumu Marekani kutaka "kuupindua" utawala wa Tehran.
"Ni jambo linalojulikana kuwa Marekani inaonesha wazi mpango wake unaolenga kupindua serikali ya Iran, na ndio maana imeendelea kusisitiza kuhusu mazungumzo," amesema Rais Rohani ambaye ameielezea msimamo wa Marekani kuwa ni "ugaidi wa kiuchumi" na kusema kurejeshwa kwa vikwazo vya Marekani ni "ukiukwaji wa haki kwa maendeleo".
Hassan Rohani amefutilia mbali wazo lolote la mazungumzo kati ya nchi yake na Marekani. Hassan Rohani,hata hivyo, amesema kuwa mazungumzo yanaweza kuendelea katika Umoja wa Mataifa.