Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:32 am

NEWS: TRUMP MBIONI KUFUTA LESENI ZA VYOMBO VYA HABARI VINAVYO MKOSOA

Washington: Rais wa Marekkani Bw. Donald Trump amesema kuwa atafutilia mbali lesini za vyombo vya habari vinavyo mkosoa , Trump ameendeleza mgogoro wake na vituo vya televisheni nchini humo akisema kuwa vimekuwa na upendeleo Tangu kuchangulia kwake kuwa Rais.

Ametolea mfano alivyokasirishwa na ripoti ya chombo cha habari cha NBC kilichoripoti aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kwamba alitaka kuongezwa kwa kiwango kikubwa silaha za kinyuklia nchini marekani.

Rais Trump alidai kuwa habari hiyo ilitungwa na hakuna ukweli juu ya hilo.

Pia Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis aliitaja taarifa hiyo kama isiokuwa ya ukweli.

Skendo ya Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita bwana Trump 'mtu mjinga' matamshi ambayo Bwana Tillerson hajayapinga lakini ambayo rais Trump ameytaja kuwa habari bandia.

Wanahabari wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufutilia mbali lesen za vyonbo vya habari.

Zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo.

Lakin baadhi ya makundi ya kupigania haki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.