Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:50 pm

NEWS: TRUMP AZITAMBUA CHINA NA URUSI KUWA TISHIO KUBWA KWA MAREKANI

Washington: Rais wa marekani Bw. Donald Trump amezitaja kuwa China na Urusi ni washindani wanaopinga ushawishi wa Marekani katika ngazi ya kimataifa.

Licha ya kuwa Marekani inaongoza kwa kuwa na jeshi lenye nguvu lakini bado wapinzani wake wa kisiasa na kiuchumi wanahangaika duniani kote ili kuitoa katika mstari.

Trump ametangaza mkakati wa kitaifa wa usalama katika utawala wake ambao unaangazia vipaumbele vya kwanza vya Marekani.

Mkakati huo umesisitiza ukuaji wa kiuchumi na usalama wa taifa hilo kwa kuweka sheria kali za kulinda mipaka na kuwa na jeshi imara.

Aidha mkakati huo unajumuisha ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Mexico, kuimarisha sheria za uhamiaji na kusitisha mpango wa kutoa viza za bahati nasibu.

Trump pia aliwakosoa pia Marais waliopita wa Marekani akisema wameshiriki katika ujenzi wa mataifa ya nje badala ya kuendeleza taifa lao .