Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:22 pm

NEWS : TRUMP ATAJWA KUWA MIONGONI MWA WANAOPIGA VITA UISLAMU

Donald Trump atangazwa kuwa nembo ya kupiga vita Uislamu mwaka 2017

Donald Trump atangazwa kuwa nembo ya kupiga vita Uislamu mwaka 2017

Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu (IHRC) yenye makao yake mjini London nchini Uingereza imemtangaza Rais Donald Trump wa Marekani kuwa ndio nembo ya propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika mwaka huu wa 2017.

Uamuzi huo umetangazwa katika mahfali ya kila mwaka cha Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ambacho hutangaza majina ya watu wanaokuwa na nafasi na mchango mkubwa zaidi katika kueneza propaganda chafu dhidi ya Uislamu na Waislamu kutokana na matamshi yao ya kiuhasama, chuki, ubaguzi na kinyongo.

Mwaka uliopita wa 2016 pia tume hiyo ya IHRC ilimtangaza Trump ambaye wakati huo alikuwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, kuwa nembo na kinara wa propaganda chafu na kupiga vita Uislamu.

Wamarekani wakiandamana kupinga sera za kibaguzi za rais wa nchi hiyo

Baada ya kushinda uchaguzi wa rais nchini Marekani, Trump amedumisha siasa zake za kupiga vita Uislamu na Waislamu na miongoni mwa hatua za kivitendo za kiongozi huyo ni kupasisha sheria inayowapiga marufuku raia wa nchi sita za Waislamu kuingia Marekani. Sheria hiyo imepingwa vikali na taasisi za kimataifa za kutetea haki za binadamu.

Wakati huo huo maelfu ya Waislamu na wanaharakati wa masuala ya kiraia na taasisi za kutetea haki za binadamu wamefanya maandamano mjini London kupinga amri ya Donald Trump inayowazuia Waislamu wa nchi kadhaa kuingia Marekani na wametoa wito a kupigwa marufuku kiongozi huyo kuingia katika ardhi ya Uingereza