- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRA YATANGAZA KUMFILISI ATAKAYEFANYA BIASHARA YA MAGENDO
Arusha: MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Imetangaza kumfilisi mfanyabiashara yeyote atakayepatikana anafanya magendo, Aidha imewaonya wafanyabiashara kujiepusha na biashara za magendo ili wasifilisiwe.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Richard Kayombo, alitoa onyo hilo jana May 25 katika Jukwaa la Fursa za Kibiashara mkoani hapa, lililoandaliwa na Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN). Aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanafanya shughuli zao salama kwa kuepuka kufanya magendo.
“Sisi tukikamata mfanyabiashara amefanya magendo tunamfilisi kama tulivyofanya siku chache zilizopita mkoani hapa, tulikamata biashara za magendo na tumefilisi malori yaliyotumika kusafirisha na kwa kufanya mfanyabiashara lazima atarudi nyuma,” alisema. Aidha, aliwaomba wafanyabiashara kujenga urafiki na TRA pale wanapokadiriwa kodi endapo hawakuridhika, wasikimbilie kufunga biashara na badala yake waende ofisini kufanya mazungumzo ili wafahamiane na kuwekeana makubaliano. “Hatutaki watu wafunge biashara na wala wafanyabiashara wasife moyo, wawe huru na TRA ili tuzungumze kwa ajili ya kuendeleza biashara zao sio kukimbilia kuzifunga cha msingi kutekeleza makubaliano, asipotekeleza atayavunja,” alisema.
Alisema TRA ingependa watu wafanye biashara kwa uhuru na hatua ya kufunga iwe ya mwisho baada ya kushindikana kabisa kwa kila hatua. Aliwaomba wafanyabiashara wadogo kuhakikisha wanajisajili na kupata Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na NIDA na kisha TRA ili wapate TIN kwa ajili ya kutambulika katika biashara zao. Alisema kwa sasa wanapanua huduma zao kwa kufungua ofisi maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, ili wananchi waweze kufikiwa kiurahisi pale wanapohitaji huduma za TRA.