- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRA YAMWAGA AJIRA 400
Ahadi hiyo ilitolewa Mjini Shinyanga na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji (pichani), wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji wa mamlaka hiyo mkoani humo.
Dk Kijaji alisema kuwa taratibu zote zimekamilika na wakati wowote nafasi za ajira zitatangazwa na kwamba nafasi hizo zimelenga kuiwezesha TRA kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi.
“Tunatambua changamoto ya uchache wa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndio maana tumeamua kuajiri wafanyakazi hao 400 ambao ni wengi kuliko kada nyingine ili tuweze kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka na hivyo kuongeza makusanyo ya kodi zinazotakiwa kwa shughuli za maendeleo nchini,”alisema.
Alisema kuwa pamoja na uhaba wa watumishi, anaamini kuwa lengo la mwaka huu la kukusanya shilingi trilioni 17 ambazo mamlaka hayo imepangiwa yatafikiwa na ikiwezekana kuzidi kwa kutumia wafanyakazi waliopo.
Dk Kijaji alitoa rai kwa wafanyakazi wa TRA kuwa waadilifu na kwamba atakayebainika kukiuka maadili yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria. Awali Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Shinyanga Jumbe Samson, alieleza kuwa mkoa wake umepangiwa lengo la kukusanya Sh bilioni 18 na kwamba wana uhakika wa kufikia lengo hilo kutokana na mikakati mbalimbali waliyojipangia, ikiwemo kusimamia ukusanyaji kodi kikamilifu katika sekta ya madini.
Kwa upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Beatus Nchota alisema kuwa mamlaka yake imejiwekea mipango ya kufungua ofisi zake kila wilaya hapa nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili lengo walilopewa la kukusanya Sh trilioni 17 liweze kufikiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, alisema kuwa Serikali mkoani humo itahakikisha kuwa TRA inatimiza malengo yake ya kukusanya kodi na kumhakikishia Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Kijaji kwamba watasimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya Serikali.