- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRA YAJA NA MBINU MPYA, KUGAWA VITAMBULISHO BIASHARA NDOGONDOGO
Morogoro: Mamlaka ya Mapato chini Tanzania (TRA) imebuni mbinu mpya itakayo wawezesha wafanyabiasha wadogo wadogo kutambulika katika kufanya kazi zao,
Jana Jumatatu May 21 Jumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 17,601 waliokuwa mkoani Morogoro wametambuliwa na hivyo watapatiwa vitambulisho maalumu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw. Elijah Mwandumbya alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu zoezi la kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho maalumu wafanyabiashara wadogo wadogo walio katika sekta isiyo rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Masika mjini Morogoro.
Mwandumbya amesema zoezi la utambuzi linafanyika kwa kupitia vikundi vya wafanyabiashara ambapo katika mkoa wa Morogoro vikundi 1851 vyenye jumla ya wanachama 17,601 wametambuliwa na watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye jina na mahali wanapofanyia biashara zao ambavyo watadumu navyo kwa miaka mitatu.