- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRA MOSHI YATEKETEZA BIDHAA ZENYE THAMANI YA SH 23 MILIONI
Moshi: Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro imeteketeza bidhaa mbalimbali za thamani ya Sh23 milioni zilizoingizwa nchini kwa Mfumo wa magendo katika mipaka ya Holili na Tarakea mjini Moshi.
Akizungumza leo Alhamisi Mei 24, 2018 meneja msaidizi kitengo cha ushuru wa forodha, Godfrey Kitundu amezitaja bidhaa hizo zilizoteketezwa leo kuwa ni chumvi, vipodozi, mafuta kula, pipi, vifungashio na vifaa vya hospitali.
Amesema TRA husimamia mapato pamoja na kudhibiti biashara za magendo na zile zisizokuwa na viwango. Amebainisha kuwa mbali na kuteketeza bidhaa hizo, pia vyombo vya usafiri vilivyotumika kusafirisha bidhaa hizo vimetaifishwa. Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Edward Mwamilawa amesema bidhaa zilizoteketezwa zipo ambazo hazina viwango kwa matumizi na ambazo hazitakiwi nchini.