Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:36 pm

NEWS: TRA KUWATOZA KODI WAFANYA BIASHARA MITANDAONI

Dar es salaam: Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka Wafanyabiashara wanaofanya biashara kupitia mitandao mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili wajiandikishe waanze kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kama wafanyabiashara wengine wote.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere leo asubuhi alipokuwa akizungumza kupitia Clouds FM kuhusu mbinu mbalimbali wanazokusudia kuzitumia ili kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya walipa kodi na kuongeza mapato.

Kamishna Kichere amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kuhojiwa na mtangazaji kuhusu uwepo wa watanzania wachache wanaolipa kodi (zaidi ya milioni 2) wakati jumla ya Watanzania wapo takribani milioni 55.

Akizungumzia mkakati wa TRA kuongeza idadi ya walipakodi, kamishna huyo amesema wameanza kuwafikia watu wanaofanya biashara mitandaoni ambao wamekidhi vigezo vya kutakiwa kulipa kodi, wawe wanalipa kodi kama wafanyabiashara wengine.

Ameeleza kuwa, wafanyabishara ambao thamani ya biashara zao ni zaidi ya shilingi milioni nne wanatakiwa kufika TRA wajiandikishe ili wapate Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) waanze kulipa kodi.

Ametahdharisha kuwa, tabia ya wafanyabiashara kulipa kodi inaweza kuwasababisha matatizo ikiwamo malimbikizo ya kodi ambayo yanaweza kupelekea biashara zao kufungwa, hivyo ni vyema wakalipa stahiki hizo kwa wakati.

Mbali na kuwafikia wanaofanya biashara kwenye miatandao, Kamishna Kichere amesema kwamba wanaendelea na utoaji wa elimu kwa wananchi, ili wafahamu umuhimu wa kulipa kodi na waone kuwa ni wajibu wao kufanya hivyo bila kusubiri kushurutishwa