- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TRA FEKI AJIKUSANYIA ZAIDI YA SH 180 BIL
Dar es salaam: Mamlaka ya mapata Tanzania TRA imemburuza mahakamani mfanyabiashara, Mustapha Kambangwa (34), mkazi wa Kongowe Mbagala, jijini Dar es Salaam kwa kosa la kujipatia pesa kiasi cha Tsh. Bilioni 188.9 kupitia mashine ya kieletroniki EFD.
Akisoma mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtenga, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa, inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo kwa siku tofauti kati ya Juni mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka huu.
Wakili Msigwa alielezea mahakama kuwa Kambangwa alijifanya kuwa amesajiliwa kukusanya kodi ya ongezeko la thamani VAT ya Sh 188,928,752,166 kwa kujifanya anakusanya fedha hizo kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika shtaka la pili kati ya Juni mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka huu, kwa udanganyifu alitumia mashine ya kielektroniki ya EFD yenye namba 03TZ842011315 iliyosajiliwa kwa jina la Kampuni ya Abraham’s Group LTD kukwepa kodi ya VAT yenye thamani ya fedha hiyo.
Katika shtaka la utakatishaji fedha, tarehe na kipindi hicho, maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, alijipatia au kujimilikisha fedha hizo alizozipata kutokana na makato ya kodi ya VAT ambazo zilipaswa kutolewa kwa Kamishna wa TRA na mshtakiwa huyo alipaswa kujua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la ukwepaji kodi.
Wakili Msigwa alidai katika tarehe tofauti kati ya Juni mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam kwa vitendo vya makusudi vya kukwepa kodi alitumia mashine ya kielektroniki ya EFD na huku akijua kwamba hajasajiliwa kama mlipakodi ya VAT aliisababishia TRA hasara ya Sh 188,928,752,166.
Alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Mtega alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi itakapopata kibali.
Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Shamo Shadrack, aliiomba mahakama kupanga tarehe ya karibu ili kupinga mashtaka hayo dhidi ya mshtakiwa.
Upande wa mashtaka ulikubaliana na hoja hiyo na kudai kuwa hauna pingamizi kwa sababu hawajui ni mapingamizi gani yatakayowasilishwa.
Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuamuru mshtakiwa kwenda rumande kwa sababu mashtaka hayo hayana dhamana.