Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:40 pm

NEWS: TPA YASEMA IDADI YA MELI ZINAZOINGIA TANZANIA ZIMEPUMGUA

Dar es salaam: Mamlaka ya Bandari (TPA) imesema idadi ya meli zinazoingia nchini imepungua kutoka 1,200 hadi 1,000 huku kwenye mfumo wa mapato yakiongezeka ambapo TPA imekusanya Tsh 728bn kwa mwaka wa fedha unaoishia june 30,2017 bandari ya Da es salaam na Kigoma ndio zinazo ongeza kwa mapato.

TPA imetoa Sababu zilizotajwa kupungua kwa meli hizo kuwa ni pamoja na uwezo wa mdogo kutia nanga kwa meli ambao hutegemea kina cha maji na kwamba kuna meli nyingi ambazo zinasubiri nje ya gati.

Kina cha maji kuna mahali ni mita saba wakati kwingine ni mita 10.5 na meli nyingi duniani ni kubwa hivyo nyingine kusababisha meli kutofika nchini.
Sababu nyingine za usalama ambapo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiibiwa hadi betri na kwamba nyingine ni usimamizi wa sera ambapo awali kulikuwa kuna baadhi ya watu wanaleta mizigo hawalipii.