- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TCRA YATOA LESENI 45 KWA WATOA HUDUMA ZA MTANDAO
Dar es salaam: Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imetoa vibali 45 kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandaoni.
Akiongea leo May 25 baada ya kutoa leseni hizo Mkurugenzi wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema 45 ndio wamekidhi vigezo kati ya waombaji 262
Aidha kabaka amesema mchakato bado unaendelea, atoa sababu kuweke gharama za usajili, pia amesema leo ni siku muhimu katika tasnia ya habari na utangazaji kutokana na kushuhudiwa wadau wa habari wakiwa wamekamilisha hatua za usajili ili watambulike na kutumia fursa hiyo ya utoaji na upashaji habari kupitia mtandao wa intanenti.
"Kutokana na kukamilisha mchakato huo TCRA imetoa leseni kwa watoa huduma wa maudhui kwa njia ya mtandao wa intanenti 45 kati ya watoa huduma 262 walioomba na kushindwa kutimiza vigezo vilivyowekwa"
amesema kuwa zipo faida nyingi za habari na utangazaji kwa njia ya mtandao ambazo zinafahamika kwa wengi. "Kama tunavyofahamu kwa miongo mingi sasa sekta ya habari na utangazaji imekuwa ikipata habari kwa njia ya redio na televisheni kupitia majukwaa mbalimbali kama mitambo iliyojengwa ardhini,Satellite na Cable.