- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TCRA YATANGAZA KUVIFUNGIA VING'AMUZI VYA DSTV NA ZUKU
Dar es salaam: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imetangaza kusudio la kusimamisha na kuzifungia leseni zilizotolewa kwa ving'amuzi vya Dstv na Zuku kwa kushindwa kutekeleza amri na masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na kuendelea kubeba/kuonesha chaneli zenye leseni za kutazamwa bila malipo yaani Bure kupitia ving'amuzi vyao
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Agosti 7, 2018 na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania inasema kuwa MULTICHOICE TANZANIA LTD imevunja sheria na imekaidi kutelekeza amri halali ya TCRA kwa kuendelea kuwatoza watazamaji wa chaneli za televisheni ambazo zinatakiwa zitazamwe na wateja kupitia ving’amuzi vyao isipokuwa TBC1 pekee bila malipo,
TCRA inautangazia Umma kuwa inakusudia KUSIMAMISHA leseni zote zilizotolewa na TCRA kwa MULTICHOICE TANZANIA LTD kwa kushindwa kutekeleza amri halali za TCRA na kwa kushindwa kutekeleza masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na kushindwa kuruhusu watazamaji kutazama chaneli ambazo zinatakiwa kutazamwa kupitia ving’amuzi vyao bila malipo.