- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TBA YASEMA NYUFA ZA MAJENGO YA UDSM NI ZAKAWAIDA SANA
Dar es salaam: Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha za majengo ya Mabweni ya chuo kikuu cha Dar es salaam zinazosambaa mitandaoni zikionyesha nyufa nikweli ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.
Akizungumza Leo Jumatatu 04.12.2017 baada ya kusambaa kwa picha za majengo hayo, Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint' ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.
Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga
"Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana Mwakalinga.
Rais John pombe Magufuli na Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga wakikagua ofisi za majengo UDSM
Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.