- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TANESCO YAWABAINI WANAO CHEZEA MITA ZA UMEME
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewabaini wahalifu wa umeme wanaochokonoa mita za umeme ili umeme usipite kwenye mita zao kupelekea kutumia umeme bila malipo.
Shirika hilo limebaini baada ya kuanza kwa operesheni na kuwanasa wachepusha umeme kadhaa eneo la Kinondoni Kaskazini.Operesheni hiyo imeanza jana ambako wateja kadhaa wamebainika kufanya vitendo hivyo vya kuchepusha umeme usipite kwenye mita kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa matumizi yake na hivyo kuliibia shirika hilo.
Kaimu Meneja wa TANESCO anayeshughulikia Wateja Wakubwa, Frederick Njavike, alikuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza
Alisema si tu wateja binafsi wanaofanya hujuma hizo lakini pia taasisi za umma likiwamo shirika moja la umma (jina linahifadhiwa).
Njavike alisema kwa kawaida kila mwisho wa mwaka shirika hupanga siku za kufanya ukaguzi wakushtukiza kuangalia sehemu gani TANESCOinapoteza mapato.
“Tumekuta kuna miundombinu ya TANESCO imechezewa na mbaya zaidi ni kwamba hata taasisi za umma zinashiriki vitendo hivyo.
“Wito wetu tunaomba taasisi zote za serikali kujaribu kupitia miundombinu yote ya umeme na vilevile kuangalia watu waliowapangishakwenye vitega uchumi vyao,” alisema.
Alisema TANESCO ni shirika la umma hivyo amewaomba wateja na wasio wateja kutoa taarifa kwa wale wote wanaochezea miundombinu kwa vile watakuwa wamesaidia shirika lao kuokoa fedha kutokana na wizi huo.
Ofisa wa Usalama wa shirika hilo, Mkoa wa Kinondoni,Mohammed Mtoro alisema zipo hatua mbalimbali ambazo TANESCO huchukua dhidi ya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kusimamisha huduma pamoja wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.