Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:28 pm

NEWS: TANESCO KUOKOA BILIONI 5.4 BAADA YA KUZIMWA MITAMBO YA DIZELI

Shirika la umeme Tanzania TANESCO sasa litaaokoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 450,108,508 zilizokuwa zikitumika kununua dizeli kila mwezi ambazo ni sawa na Bilioni 5.4 kwa mwaka.

TANESCO iliwasha rasmi kituo kipya na
cha kisasa cha kupoza na kusambaza umeme cha Madaba, septemba mwaka huu ambacho kimeunganishwa
kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuondoa matumizi ya umeme wa mafuta kwenye
Halmashauri ya Manispaa ya mji wa Songea na vitongoji vyake.

moja ya mitambo iluyokuwa ikifua umeme wa mafuta (dizeli) songea

Kuwashwa kwa mtambo huo ni baada ya kukamilika kwa Mradi
wa umeme wa Makambako-Songea ambao ulihusisha ujenzi wa vituo vya kupoza na
kusambaza umeme vya Makambako na Songea sambamba na upanuzi wa kituo cha kupoza

Hili ni tenki la kuhifadhia mafuta ya dezeli

na kusambaza umeme cha Makambako, lakini pia Ujenzi wa njia kuu ya
usafirishaji Umeme wa kilovoti 220 yenye urefu wa kilometa 245 kutoka Makambako
hadi Songea kupitia Madaba. Usambazaji Umeme wa msongo wa 33kV zenye urefu wa
kilomita 900 na kuunganisha wateja 22,700 katika Wilaya za Njombe , Ludewa na
mji wa Makambako katika Mkoa wa Njombe, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo
na Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma.