- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAMISEMI YAJIPANGA KUPUNGUZA VIFO VYA AKINA MAMA NA WATOTO.
DOM: Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imeweka mikakati ya kuhakikisha inapunguza vifo vya akina mama na watoto vitokanavyo na uzazi sababu kutoka 556 hadi 292 kwa vizazi hai laki moja ifikapo mwaka 2020. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2015/2016 ulionyesha kuwa idadi ya vifo vya akina mama iliongezeka kutoka 454 hadi 556 kwa vizazi hai laki 1. Mkurugenzi wa Huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Tamisemi dokta Ntuli Kapologwe ameyaeleza hayo jana ofisini kwake jijini hapa wakati akizungumza na mtandao huu Amesema dhamira yao hasa ni kutoona kifo chochote cha akina mama na watoto kinatokea kwa ajili ya uzazi au sababu nyingine lakini wana amini kuwa wanaelekea katika njia sahihi ya kutokomeza vifo hivyo. Hata hivyo amesema ili dhamira hiyo ifanikiwe wamekuwa wakifanya ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na ujenzi wa zahanati mpya na kutolea mfano mwaka 2017/2018 wamejenga zahanati zipatazo 183,wamefanya ukarabati wa vituo vya afya vipatavyo 518 lengo likiwa ifikapo 2020 kuwe na vituo vya afya 888. “Ili kufikisha idadi hiyo kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2020 tutahitajika kujenga vituo vya afya 289 na hivyo kufikia asilimia 20 kwa sababu kata zilizopo nchini ni elfu 4,420 na kutokana na Sera ya Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) tunatakiwa kujenga kituo cha afya kwa kila kata,”ameongeza dokta Kapologwe. Akiendelea kufafanua amesema jitihada hizo kwa sasa wanafanya uimarishaji wa mifumo ya rufaa ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2019 wanajenga Hospitali za Halmashauri 67 na tayari zimetengwa shilingi bilioni 100.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hizo 67 ambapo kila hospitali moja itagharimu shilingi bilioni 1.5 kwa awamu ya kwanza. “Haya ni mafanikio makubwa,tunaamini uwepo wa vituo vyetu vya afya, ambavyo tunatarajia ifikapo mwaka 2020 vifikie 888 (20%) na uwepo wa hospitali 67,uwepo wa hospitali nyingine za serikali 77 na uwepo wa hospitali za mashirika ya dini (FBOs) 38 itasaidia kuimarisha mfumo wa rufaa nchini na kupunguza umbali mrefu wa akinamama kwenda kufuata huduma na hivyo kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi,”amesema dokta Kapologwe. Ametaja mikakati mingine kuwa mpaka hivi sasa Serikali imeweza kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wapatao elfu 11,500 ambao watapelekwa katika vituo vya afya vilivyoboreshwa,vinavyotoa upasuaji wa dharura na Zahanati mpya 183 ili huduma kusogezwa Mikakati hiyo inafanyika kwa kuongozwa na nyaraka mbalimbali ikiwemo mkakati wa nne wa sekta ya afya ambao unaelekeza nini kifanyike ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto vitokanavyo na uzazi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ilikyoweka dhamira ya kupunguza vifo hivyo |