- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAJIRI WA ALIBABA ATANGAZA KURUDI KWENYE KAZI YA UWALIMU
Gazeti mmoja nchini Marekani la New York Times limemnukuu Mmoja wa watu matajiri zaidi nchini China na Duniani kwa ujumla wake Jack Ma,amesema ataacha wadhifa wake kama mwenyekiti mkuu wa kampuni ya yake ya bishara ya mtandaoni Alibaba na kurudi kwenye fani yake ya uwalimu.
"Kuna vitu ninaweza kujifunza kutoka kwa Bill Gates," alisema
"Sitaweza kuwa tajiri kama yeye, lakini kitu kimoja ambacho nitaweza kufanya ni kustaafu mapema. Nafikiri siku moja nitarudi kuwa mwalimu. Hiki ni kitu ninaamini nitafanya bora zaidi kuliko kuwa mkurugenzi wa Alibaba."
Bwana Ma alianzia taaluma ya ualimu akifunza luhgha ya kiingerza katika chuo kikuu huko Hangzhou mashariki mwa mkoa wa Zhejiang. Alanzisha kampuni ya ya Alibaba kutoka nyumbani kwake huko Hangzhou.
Hata hivyo atabaki kwenye bodi ya wakurugenzi lakini atakuwa anaangazia masuala ya utoaji misaada na elimu, kwa mujibu wa gazeti la New York Times.
Bw Ma alianzisha kampuni ya Alibaba mwaka 1999 na ameiongoza hadi kufikia kuwa moja ya kampuni kubwa zaidi duniani.
Ikiwa na thamani ya dola bilioni 400 Alibaba uhusika na mambo yakiwemo uuzaji ya bidhaa mitandano, uzalishaji wa filamu na kuhifadhi nyaraka.
Mwalimu huyo wa zamani wa lugha ya kiingereza anasema kustaafu sio mwisho wa mambo bali sasa ndio mwanzo, akiongeza kuwa "ninapenda elimu".
Bw Ma ambaye atafikisha umri wa miaka 54 siku ya Jumatatu, ana utajiri wa dola bilioni 40 na kumfanya kuwa mtu wa tatu tajiri zaidi nchini China.
Mapema wiki hii Bw Ma alikiambia kituo cha Bloomberg kuwa anataka kuanzisha wakfu kufuata nyayo za tajiri wa Microsoft, Bill Gates.