- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : TAARIFA ZILIZOBEBA UZITO ALFAJIRI YA LEO OCT 27.2017
Umeamkaje ! Karibu katika uwanja wa habari,na tuangazie taarifa zinazochukua nafasi kubwa alfajiri ya leo,tuaambiwa kuwa
-Tume ya uchaguzi Kenya yaahirisha uchaguzi katika majimbo 4
Kwa Ufupi
Uchaguzi utarudiwa tarehe 28 mwezi huu katika Maeneo manne kutokana na machafuko ambayo yalitokea. Mwenyekiti wa Tume ya Kusimamia Uchaguzi amesema kaunti zilizoathirika ni Siaya, Migori, Kisumu na Homa Bay
-Tukibakia Nchini Kenya,Watu kadhaa wauawa na makumi wajeruhiwa katika uchaguzi wa marudio wa urais
Taarifa inasema,Watu wasiopungua wanne wameuawa katika mkoa wa Nyanza na mji wa Machakos nchini Kenya katika ghasia za uchaguzi wa marudio wa rais uliofanyika jana nchini humo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya watu wawili waliuawa wakati polisi walipopambana na wapinzani wa marudio ya uchaguzi wenye mfungamano na muungano wa upinzani wa NASA huko Kisumu na Homa Bay jana
-Kwengineko,Nchini Burundi,Serikali yaunga mkono marekebisho ya katiba
Serikali ya Burundi imeidhinisha marekebisho ya katiba ambayo yatatoa fursa ya kurefushwa kwa uongozi wa Rais Pierre Nkurunzinza, kulingana na maelezo ya maafisa waandamizi wa serikali hiyo,Huenda uongozi wa rais Pierre Nkurunzinza ukarefushwa kwa miaka mingine 14. Hii ni baada ya serikali ya Burundi inayokabiliwa na migogoro kuidhinisha marekebisho ya katiba ambayo yatatoa fursa ya kurefushwa kwa uongozi wake, kulingana na maelezo ya viongozi wakuu.