- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA ZA MKUU WA WILAYA KUMPIGISHA MAGOTI AFISA MTENDAJI
Mkuu wa wilaya ya Bunda bi. Lidya Bupilipili amemuamrisha Afisa Mtendaji wa kata ya kitengule wilaya ya bunda ndg. Deus Bwire kupiga magoti mbele ya viongozi wenzake kwenye kikao.
Bi Lidya mkuu wa wilaya Bunda
Bi Lidya amefanya tukio hilo Jana Oct. 2, 2018 ambapo mkuu huyo aliwataka watendaji wa vijiji ambao hawakuudhuria kikao waripoti kesho yake ofisini kwa mkuu wa wilaya.
Baada ya Agizo hilo Bw. BWIRE alisimama na kumuelezea Mkuu huyo sababu ya watendaji hao kutofika kwa wakati huo, kuwa walichelewa kupata taarifa ndiyo maana hawakuudhuria katika kikao hicho.
Sasa muda mchache Baada ya maelezo hayo mkuu wa wilaya hakuridhishwa nayo na akamtaka mtendaji huyo kupiga magoti mara moja, "Hebu piga Magoti kwanza" aliamuru Bi Lidya kitendo ambacho Bw. Bwire alitii kwa muda wa nusu saa akiwa amepiga magoti na baadae akaruhusiwa kuinuliwa.
"Mimi Nina miaka zaidi ya hamsini na nina watoto tisa na wajukuu,lakini kitendo cha kupigishwa magoti mbele ya kundi la viongozi wenzangu kama mtoto wa darasa la pili ni kunidhalilisha na hadi sasa sipo sawa alisema Ndugu Bwire baadae muda mchache baada ya kuamriwa.
“Taratibu za kazi zifuatwe na mimi nipo tayari kujiuzulu lakini sipo tayari kudhalilishwa kama nilivyodhalilishwa utadhani nimeiba au nimetumia mali ya Serikali vibaya, Rais aangalie hali kama hizi” Ofisa Mtendaji huyo.