Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:28 am

NEWS: TAARIFA ZA KUKAMATWA MDOGO WA BILIONEA NAMBA 2 TANZANIA

Dar es Salaam: Mfanyabiashara Akram Azizi ambaye anatambulika kama Mdogo wa Bilionea maarufu nchi Rostam Azizi amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi, ikiwamo kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji wa fedha ambazo ni Dola za Kimarekani $9,018.

Image result for rostam azizi

Akrzm baada ya kukamatwa leo Octoba 31, 2018 anakabiliwa na mashtaka 70 ya kukutwa na silaha, mawili ya kukutwa na risasi, mawili ya kukutwa na nyaraka na moja la utakatishaji wa fedha.

Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali wakuu, Paul Kadushi na Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12, 2018.

Inataarifiwa kuwa Akram ni Mdogo wa bilionea Rostam Azizi ambaye Jarida la Forbes lilimuweka nafasi ya kwaza mwaka 2015/2016 kuwa mtu mwenye utajiri mkubwa zaidi nchini Tanzania akiwa na utajiri unaokadiriwa kuwa ni dola za kimarekani Bilioni $1.1 nasasa tajiri huyo anashika nafasi ya pili Nyuma ya Bilionea Mohamed Dewji 'MO' Mwenye utajiri wa dola za kimarekani Bilioni $ 1.4

Image result for rostam azizi