- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA ZA KUKAMATWA KWA MTANGAZAJI SHAFII DAUDA
Dar es Salaam: Taarifa kutoka jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wanasema wanamshikilia mtangazaji wa wa michezo wa kituo cha televisheni cha Clouds, Shaffih Dauda na mwenzie MC Luvanda kwa kosa la kumiliki mitandao ya Youtube bila kusajili maudhui yake mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA
Mwingine aliyekamatwa katika sakata hilo ni pamoja na msimamizi wa mtandao wa Youtube wa Shaffih, anayejulikana kwa jina Ben Ali, maarufu kwa jina la Ben On Air.
Taarifa kutoka kwa kamanda Mkuu wa kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amedhibitisha kuwa Jana Septemba 18, wanamshikilia Shaffih na wenzake kwa makosa ya kimaudhui mtandaoni.
Lakini taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa Shaffih zinadai mtangazaji huyo na wenzake hao walikamatwa tangu Ijumaa iliyopita na kufikishwa kituo cha polisi cha Mabatini kabla ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi wanakoshikiliwa hadi sasa.