- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA ZA KUKAMATWA KWA MBUNGE BWEGE
KILWA: Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara maarufu kama 'Bwege' anashikiliwa na Jeshi la polisi akidaiwa kutaka kufanya mkutano wa hadhara bila kuwa na kibali.
Kwamujib wa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai amedhibitisha kuwa ni kweli jana usiku Oktoba 1, 2018 Bwege na wenzake walikamatwa saa 10 jioni eneo la Maalim Seif lililopo Kilwa Kivinje kwa kosa la kukaidi amri ya Jeshi la Polisi Wilayani Humo lakini aliachiwa baada ya saa 2 baadae.
Ngubiagi amesema wanaoshikiliwa na polisi ni madiwani wanne akiwemo diwani wa Kilwa Masoko na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka.
"Bungara alipeleka barua ila kwa sababu za kiusalama polisi walizuia mkutano huo na yeye aliomba asiufanye. Endapo angefanya kungekuwa na uvunjifu wa amani," amesema Ngubiagai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo
Kabla ya kumkamata kwake inadaiwa waliwatawanya wananchi kwa mabomu na kuvunja mkutano wake.