- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA YA WAFANYAKAZI WA TANESCO KUFYEKWA POSHO ZAO
Dar es salaam: Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema fedha za posho ambazo huwa wanapokea wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zitatumika katika ununuzi wa mashine ili kuwezesha wananchi kupata umeme.
"Safari za ndani na nje tutazipunguza tutaelekeza fedha kwenye mashine. Shirika hili linaweza kujiendesha vizuri. Pamoja na matatizo ya kifedha tuliyonayo kuna fedha sisi watumishi tunapata zitakwenda kwenye mashine,” amesema.
Kalemani amesema, “Tutakapopungukiwa tutaomba taasisi nyingine lakini awali ya yote nimeamua posho za wafanyakazi, semina na mimi mwenyewe zitakwenda kwenye mashine tusipate shaka kupata fedha ya kununua mashine."
Dk Kalemani amesema hayo leo Jumatatu alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Mtwara.
Amewahakikishia wakazi wa mji wa Mtwara kuanzia sasa tatizo la umeme halitakuwepo.
Kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi na Mtwara, amesema jitihada zinaendelea ili kupata suluhisho la kudumu hadi ifikapo Novemba.
Waziri Kalemani amesema Serikali inayafanyia kazi matatizo ya kukosekana umeme wa uhakika katika mikoa hiyo.
Amesema leo Jumatatu zitapatikana megawati mbili na kufanya idadi ya umeme unaozalishwa kuwa megawati 12, hivyo kupunguza makali ya mgawo.
"Umeme unawaka hautazimika tena kwa Mtwara mjini kuanzia leo. Zipo mashine tisa na zinazofanya kazi sasa ni nne ambazo zinatoa megawati nane, juhudi zinaendelea kurekebisha mashine mbili na leo zitakamilika na tutakuwa na megawati nyingine nne hivyo kuwa na jumla ya megawati 12," amesema Dk Kalemani.