- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA YA KUJIUZULU KWA VIGOGO WA ACACIA
Dar es salaam: Kampuni inayojihusisha na Uchimbaji wa madini Tanzania ACACIA imekumbwa na pigo kubwa baada ya kutangaza kujiuzulu kwa maafisa wake wakubwa wa ngazi ya ya juu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Brad Gordon na Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray wamejiuzulu nyadhifa zao leo Alhamisi Novemba 11, 2017. Taarifa kutoka Acacia zimeeleza
Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema kuwa anataka kurudi nyumbani Australia kusimamia masuala ya familia yake wakati Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray akisema amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine.
“Pamoja na uamuzi huo, wote wataendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo wakati wakikabidhi majukumu ya ofisi kwa warithi wao,” imesema taarifa ya Acacia iliyotolewa leo Alhamisi asubuhi.
Mnamo Oktoba 19, Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold Mine inayomiliki asilimia 63.9 ya hisa za Acacia ilitangaza makubaliano yaliyoafikiwa baada ya majadiliano ya takriban miezi mitatu ambapo kampuni hiyo ilikubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya za madini pamoja na kulipa Dola 300 milioni za Marekani wakati majadiliano kuhusu kodi yakiendelea.
Oktoba 20, Wray aliwaambia waandishi wa habari kwamba Acacia haina uwezo wa kulipa kiasi hicho kwa mkupuo.