- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA YA KUJIUZU KWA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRMAN KINANA
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amemwandikia barua Mwenyekiti wa chama hicho ambaye ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, akimwomba kujiuzulu wadhifa wake huo.
Kinana ambaye amekuwa Katibu Mkuu wa CCM tangu mwaka 2012, taarifa ambazo tumezipata kutoka katika watu wake wa karibu wa mwanasiasa huyo, zinadai mwenyekiti wao Rais Magufuli ameridhia ombi lake hilo baada ya kumkakatalia huko nyuma.
Taarifa zinaeleza Kinana anatarajiwa kutangaza uamuzi wake wa kujiuzulu kesho wakati vikao vya juu vya chama hicho kwa maana ya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vitakapoanza kuketi, Ikulu, Dar es Salaam.
Julai 2016, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ambao Rais mstaafu Jakaya Kikwete alimkabidhi uenyekiti wa CCM Rais Magufuli, ikiwa ni miezi minane tangu aingie madarakani, Kinana aliwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo, lakini kiongozi huyo wa nchi aliikataa akimwomba amsaidie kwa sababu ya uzoefu wake.
Rais Magufuli, pia aliwataka manaibu katibu wakuu wawili na sekretarieti nzima ya chama hicho, kuendelea na kazi.
Watu wake wa karibu wanasema kuwa uamuzi wa Kinana kuomba kuondoka katika nafasi hiyo, unatokana pamoja na sababu kuwepo kwa mambo ambayo hashirikishwi.
Inaelezwa miongoni mwa mambo ambayo Kinana anaona hakushirikishwa kwa nafasi yake na amepata kusikika akisikitika kwa watu wake wa karibu, ni suala zima la uundwaji wa kamati kuchunguza mali za CCM.
Tayari ripoti ya kamati hiyo ilikabidhiwa kwa Rais Magufuli hivi karibuni na kimsingi huenda ikajadiliwa na wahusika kuchukuliwa hatua katika vikao hivyo vinavyoanza kuketi kesho.
Jambo jingine ni uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo ya Siha na Kinondoni, ambalo wana CCM wengi pia walilamika kuwa utaratibu wa chama hicho ulikiukwa.
Hata kabla ya Kinana hajaomba kujiuzulu, mjadala wa yeye kuondoka kwenye nafasi hiyo licha ya kudumu kwa muda mrefu na hata wakati fulani kutulia, ulirejea tena kwa kasi juzi na jana baada ya Rais Magufuli kuonekana akifanya vikao bila yeye kuwapo.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Mangula.
Pasipo kufafanua, taarifa hiyo ilieleza viongozi hao wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu CCM na Serikali.
Juzi, Rais Magufuli alikutana na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Mangula, na kufanya mazungumzo ambayo ajenda yake haikuwekwa wazi.
Wakati zikiibuka taarifa za Kinana kuondoka sasa licha ya tetesi zake kudumu kwa muda mrefu kutokana na kutoonekana sana kwenye shughuli nyingi za CCM, tayari kulishazuka mjadala wa nani atakuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kikongwe barani Afrika.
Katika mjadala huo, licha ya kwamba jina la Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba liliwahi kutajwa, lakini kitendo cha Rais Magufuli kukamilisha nafasi mbili za uteuzi wa wajumbe wa NEC kikatiba kwa kuwateua Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na kada wa CCM, ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere, kumeongeza namba ya watu wanaotajwa kumrithi Kinana.