- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUARISHWA KWA MNADA WA TANZANITE
Wizara ya Madini inatoa taarifa kwa umma kuwa Mnada wa Madini ya Tanzanite uliokuwa ufanyike katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara kuanzia tarehe 12 hadi 15 Oktoba, 2017, umeahirishwa hadi hapo utakapotangazwa tena.
Sababu za kuahirishwa kwa mnada huo ni kuridhia maombi ya wadau wa mnada ambao waliomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa wingi.
Aidha, uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Mererani.
Hivyo, Wizara ya Madini inawaomba radhi wadau wote wa Sekta hii ndogo ya madini ya vito hususan Tanzanite ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini