Sumaye ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi jimbo la Ukonga ametoa kauli hiyo jana Septemba Mosi, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa wao sio sehemu ya wafanya fujo lakini wanatoa tahadhari.
Sumaye ameongeza kuwa tume isiwe sehemu ya kuingiza watu kwenye matatizo, "Tunataka tume iwe huru isiogope kufanya kazi yao kwa ufasaha kwa sababu ya vitisho, sisi tunawahakikishia wananchi kuwa watadumisha amani na tutapokea matokeo kwa moyo mkunjufu ili mradi yawe ya haki”.
Uchaguzi mdogo wa marudio katika majimbo ya Korogwe Vijijini mkoani Tanga, Monduli jijini Arusha na Ukonga jijini Dar es salaam unatarajiwa kufanyika Septemba 16 baada ya mbunge mmoja kufariki na wengine wawili kujiuzulu