- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: STEVE NYERERE ATENGWA KWENYE MSIBA WA MZEE MAJUTO
Dar es Salaam. Chama cha Waigizaji taifa kwa kushirikiana na chama cha waigizaji Kinondoni vimemuweka kando Muigizaji Steve Nyerere kwenye msiba wa Mzee majuto ambaye amekua mstari wa mbele kuwaunganisha wasanii wenzake hasa katika kipindi cha misiba au matatizo yanayowatokea wasanii wenzao.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuundwa kamati ya kushughulikia msiba huo ambayo imeundwa na Chama cha waigizaji Mkoa wa Kinondoni (TDFAA) pamoja na chama cha waigizaji Taifa.
Kuondolewa kwa Steve ni kutokana na kutokuwa mwanachama wa TDFAA hivyo hawezi kuteuliwa katika kamati.
Hata hivyo nae kwa upande wake steve Nyerere jana alionesha msimamo wake wa kutoshiriki kikamilifu kwenye msiba huo kwa sababu ya namna ambavyo watu wamekuwa wakimchukulia kwenye shughuli kama hizo
"nimeshasema siongei kitu, kuna viongozi wanaofatilia hii,nimeshatukanwa sana , nimeshasemwa sana,nimefedheshwa sana, na mimi pia nina familia na nina watoto pia kwaio mimi sio msemaji mkuu lakini nia ni kumpumzisha mzee lakini mimi iswezi kusema chochote kile.mimi ni muombeleza kama waombelezaji wengine" alisema Steve
Mara baada ya Mzee Majuto kufariki, wajumbe wa kamati wakiongozwa na Simon Mwakifamba walifika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya taratibu za kuhifadhi mwili na wakatoa tamko kwamba taratibu zote za kuaga zitafanyika Muhimbili na baadaye kusafirisha kwenda Donge, jijini Tanga kwa mazi