Akizungumza kwa njia ya simu kwenye kipindi cha East Afrika Breakfast, kinachorushwa na East Afrika Radio, Spika Ndugai amesema ni vema akatafutwa mke wake ili aelezee namna ambavyo Bunge limejitahidi kumtunza Marehemu, Tangu akiwa Dodoma, ikiwemo kusimamia gharama za matibabu yake pamoja nakumtunza mke wake.
“Mimi nafikiri mumtafute mke wake, yeye ndio anaweza kuwaeleza ana shukrani kiasi gani kwa Bunge, ambao ndio tumemtunza tangu anaugua kule Dodoma, ambao ndio tumelipa gharama zote za matibabu, ambao ndio tumekodisha ndege kutoka Dodoma kumleta Dar es salaam mpaka Muhimbili, ambao ndio tumemtunza Muhimbili muda wote, mpaka amefariki mikononi mwetu tukiwa tunamtunza mgonjwa na mke wake, ukishafanya yote hayo halafu mtu mwishoni anakuja , yaani hakuwepo alikuwa nje ya nchi, anasema kwamba wewe hakuna ulichokifanya, sasa wewe ujibuje, siuseme tu Haleluya Inatosha.” Alisema Spika Ndugai.