- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SPIKA NDUGAI AMTIMUA BUNGENI MBUNGE WA CHADEMA MWINGINE
Dodoma: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemfukuza Mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga ndani ya bunge kwa madai ya kufanyiwa utovu wa nidhamu.
Ndugai amechukua uwamuzi huo baada ya kukaa kwa muda kiasi akitoa amrikwa vyombo vya ulinzi vimsaidie kumpata mbunge aliyefanya utovu wa nidhamu wakati mbunge wa Tandahimba (CUF) Katani Ahmed Katani alipokuwa akitoa mchango wake.
Katani ameanza kwa kukanusha madai ya kujiuzulu akisema vyombo vya habari havikumtendea haki ndipo wabunge wa upinzani wakaanza kupiga kelele lakini Spika alipowanyamazisha wakaanza kuzomea.
"Nimejiridhisha kupitia vyombo vyangu, aliyefanya utovu wa nidhamu ni mheshimiwa Susan Kiwanga, sasa nakuomba utoke nje hadi bunge lijalo tutaonana Mungu akipenda Januari mwishoni mwakani," amesema Spika Ndugai
Amemtaka mbunge huyo kutojihusisha na vikao au kamati za Bunge katika kipindi hiki na kuwa kama alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa Bunge anapaswa kuondolewa jina lake.
Susan anakuwa ni mbunge wa pili Katika mkutano wa 13 baada ya jana Jumatano Mbunge wa Iringa Mjini (Chaden) Mchungaji Peter Msigwa kufukuzwa na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kuambiwa alikuwa anapiga kelele.