- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SOPHIA SIMBA ALIYEFUKUZWA NA CCM APEWA CHEO NA RAIS MAGUFULI
Dar es salaam: Aliyewahi kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto Sophia Simba, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa Ustawi wa Jamii.
Simba ambaye alifukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kukisaliti chama chake, kabla ya kusamehewa na kurudishwa kwenye chama mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais John Magufuli amewateua wenyeviti wengine wanne wa Bodi za taasisi za serikali baada ya waliokuwa wakiongoza bodi hizo kumaliza muda wao na wengine kuteuliwa katika nyadhifa nyingine.
Katika uteuzi huo, Profesa Anael Mkonyi, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mifupa (Moi), Mwamini Juma kuwa Mwenyekiti Bodi ya Sukari na Dk. Mwanza Kamata kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Christopher Chiza ambaye amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Buyungu.
“Rais Magufuli pia amemteua Dk. Maria Mashingo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo (TIB) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Palamagamba Kabudi ambaye aliteuliwa kuwa Waziri na baadaye kuwa Waziri wa Katiba na Sheria,” imesema taarifa hiyo.
Bi Simba alifukuzwa uwanachama wa CCM March 11, 2017 kwa madai ya kukisaliti chama pamoja na Dkt. Emanuel Nchimbi wengine ni Wenyeviti wa Wilaya wa CCM
- Omary Awadhi- Mwenyeviti wa Wilaya ya Gairo -Amefukuzwa uanachama
- Ally S. Msuya- Mwenyeviti wa Wilaya ya Babati Mjini -Amefukuzwa uanachama
- Makoi S Laiza -Mwenyeviti wa Wilaya ya Longido.
- Abel Kiponza -Mwenyeviti wa Wilaya ya Iringa Mjini – ameachishwa uongozi
- Salum Kondo Madenge – Mwenyeviti wa Wilaya ya Kinondoni – amefukuzwa uanachama
- Assa Simba Harun –Mwenyeviti wa Wilaya ya Ilala – Ameachishwa uongozi uanachama
- Wilfred Ole Morel – Mwenyeviti wa Wilaya ya Arusha Mjini – Amefukuzwa uanachama
- Hamis J. Nguli- Mwenyeviti wa Wilaya ya Singida Mjini- Ameachishwa uongozi.
- Muhaji Bishako – Mwenyeviti wa Wilaya ya Muleba -Amepewa onyo kali
Viongozi wa Jumuia Waliopatikana na makosa
Josephine Genzabuke – Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Mkoa wa Kigoma – amepewa onyo kali.
Sophia Simba – Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa – amefukuzwa uanachama.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Emmanuel Nchimbi—Mjumbe Kamati Kuu – alipewa onyo kali, akatakiwa kuomba radhi wanachama, uongozi na Chama Cha Mapinduzi kwa makosa ya kiuadilifu aliyotenda aliyotenda, atatakiwa aombe radhi huko huko aliko Ubalozini nchini Brazil.
Adam Kimbisa – Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma