- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : SIO SIRI TENA YADAIWA SAUDIA NA ISRAEL ZINATAKA KUANZISHA VITA YA AFRIKA YA KATI
Siri yafichuka, Saudia na Israel zinataka kuanzisha vita Mashariki ya Kati
Imebainika kuwa, utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel zinapanga njama ya kuanzisha vita katika eneo la Mashariki ya Kati.
Barak Ravid, ripota mwandamizi wa masuala ya kidiplomasia wa televisheni ya Israel ya Channel 10 News amechapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter taarifa iliyovuja kuhusu mpango wa Israel na Saudia kuzusha fitna na vita katika eneo hili.
Taarifa hiyo iliyovuja ya kidiplomasia ni waraka ulioandikwa na utawala wa Kizayuni kwenda kwa mabalozi wake wote kote duniani, ukiwataka 'wafanye kila linalowezekana' kuishinikiza Iran na harakati ya Hizbullah ya Lebanon, na kudai kwamba Lebanon imetangaza vita dhidi ya utawala wa Aal-Saud.
Kwa mujibu wa Nosratollah Tajik, balozi wa zamani wa Iran nchini Jordan, hatua ya Saudia ya kuibua mtikisiko wa kisiasa usio na maana nchini Lebanon ni ithibati ya kwanza kwamba utawala wa Riyadh unafanya kazi bega kwa bega na utawala haramu wa Israel, kueneza chuki dhidi ya Iran na Hizbullah kwa lengo la kutaka kuanzisha vita Mashariki ya Kati.
Tayari Saudia na Kuwait zimewataka raia wao waondoke nchini Lebanon haraka iwekezekanavyo.
Huku hayo yakirifiwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir ameibuka na kudai kuwa hali mbaya inayoikabili Lebanon kwa sasa ni matokeo ya hatua za harakati ya Hizbullah kupora madaraka ya Lebanon chini ya uungaji mkono wa Iran.
Jumamosi iliyopita, Saad Hariri akiwa mjini Riyadh tena chini ya mashinikizo ya utawala wa Aal-Saud, alitangaza kujiuzulu cheo cha Waziri Mkuu wa Lebanon; ambapo alitoa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na harakati ya Hizbullah.