- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SILINDE ALAANI KITENDO CHA LISSU KUPIGWA RISASI
DODOMA: Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde amelaani vikali vitendo vinavyoendela vya kupigwa kwa risasi na kuonewa kwa viongozi nchini.
Ameyasema hayo wakati wa akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2018/19 na muongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka huo
Amesema uonevu unaondelea nhini kwa baadhi ya viongozi ni hatari kwa maana unaweza kuhatarisha amani nchini.
Kauli hiyo imekuja baada ya miezi michache iliyopita mbunge wa singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma wakati vikao vya bunge vikiendelea.
Amesema toka mbunge Tundu lissu Kupinga risasi hakuna hatua yoyote iliyochuliwa na serikali kuhusiana na tukio hilo .
Aidha ametoa wito kwa waumini wa madhehebu ya dini zote kuendelea kuwaombea waathirika wote wa matukio hayo ili mungu aendelee kuwarehemu na kuwatia nguvu.
Aidha amesema ili kuendelea kulinda amani na utulivu lazima vitendo vya ubanguzi na uonevu kuachwa mara moja.