- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SIDO DODOMA YATAKIWA KUJENGA KONGANO LA UCHAKATAJI WA NGOZI
DODOMA: Naibu Waziri Wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amelitaka shirika la Viwanda vidogo vidogo (SIDO) kuhakikisha ndani ya miaka miwili linakamilisha ujenzi wa eneo maalum lililopo manispaa ya Dodoma Zuzu lililotengwa kwa ajili ya mafunzo ya uchakataji wa ngozi
Agizo hilo amelitoa leo mjni hapa alipokuwa akifanya ziara ya kikazi ya kutembekea miradi mbalimbali inayosimamiwa na Viwanda cha sido.
Manyanya amelitaka shirika hilo kuongeza jitihada katika kuhakikisha wanapanga mipango ya muda mfupi na kuachana na mipango ya muda mrefu ambayo inaonekana kupoteza muda.
" Nahitaji mchaka mchaka katika wizara yangu lazima tufanye vitu vinavyoleta mapinduzi hivyo mapambano juu ujenzi Wa Viwanda cha ngozi," amesema Manyanya.
Aliendelea " Mbona maeneo mengine wanaweza lazima na sisi tuweze vitu vya ngozi na mahitaji yake yanaeleweka," Amesema.
Awali akiongea kwa Naibu Waziri huyo Mkurungezi idara ya maendeleo ya Viwanda wizara ya Viwanda ,biashara na uwekezaji,Obadia Nyagiro amesema kuwa wazo la ujenzi huo lilikuwepo tangu mwaka 2014 kujenga kongano hilo kwaajili ya uchakataji Wa ngozi kuanzia hatua ya awali hadi ya mwisho.
Aidha amesema eneo hilo lenye hekta 107 lililopo zuzu Manispaa ya Dodoma linahitaji kuwekewa miundombinu kwaajili ya kuliendeleza.
Amesema nijukumu la Serikali kuweka miondombinu kwenye eneo hilo ili kukamilisha ujenzi wa kongano hilo.
" Tunaamini kwamba eneo likikamilika litawavutia wawekazaji mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali '', amesema.