- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHULE YA MSINGI CHIDETE YAIBUA HOJA KWA VIONGOZI WA HALMASHAURI
BAHI DODOMA: Halmashauri ya wilaya ya Bahi imeiwekea miakakti shule yake ya msingi ya Chidete iliyoshika nafasi ya mwisho kimkoa na kiwilaya .
Shule hiyo pia kitaifa ipo kwenye shule kumi duni ambapo kati ya shule 10,090 ,shule hiyo imeshika nafasi ya 10,082.
Hayo yameelezwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Leo Mavika katika kikao cha baraza la madiwani wilayani humo kufuatia swali la diwani wa kata ya Makanda Marki Mazengo kuhoji mkakati wa halamshauri wa kupeleka mwalimu wa kike kutokana na shule hiyo kutokuwa na mwalimu wa kike hata mmoja kati ya walimu watatu waliopo.
Vile vile diwani huyo amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba za walimu na upungufu hali aliyosema inaweza kuchangia wanafuzni katika shule hiyo kufanya vibaya katika mitihani yao ya Taifa.
“Nilitembelea shuleni hapo na nilipata malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa kike kwamba hawana mwalimu wa kike ambaye ataweza kuwahudumia wanapokuwa na shida,lakini shule hiyo ina walimu watatu tu kati ya walimu watano wanaohitajika.”amesema Mazengo
Akijibu Mkurugenzi amesema,shule hiyo haipaswi kuangaliwa katika suala moja tu la kupata mwalimu wa kike isipokuwa inapaswa kuangaliwa katika suala zima la kuhakikisha pia inaongeza ufaulu wake.
“Tunatamani shule hiyo ipate mwalimu hata mmoja wa kike kati ya walimu watatu waliopo kwa sasa ,lakini miakakti iliyopo ni kuhakikisha tunaangalia vikwazo vyote vinavyosababisha shule hiyo kushika mkia kwenye matokeo yake.”amesema Mavika
Aidha alisema, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 211 na kwamba wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba katika shule hiyo ni wanafunzi 37 ambapo kati ya hao waliofaulu ni watatu na kwamba Kitaifa imekuwa ya 10,082 kati ya shule 10,090 na kiwilaya na kimkoa imeshika nafasi ya mwisho.
Hata hivyo amesema mikakati waliojiwekea ili kupandisha ufaulu wa shule hiyo ni pamoja na kuhamishia baadhi ya walimu shuleni hapo wakiwemo wanawake,lakini pia lazima kuwe na usimamizi wa walimu ili kuhakikisha wanafundisha lakini pia kuboresha mazingira ya walimu ya kufanyia kazi.
Licha ya hayo ameendelea kusema Vile vile alisema lazima itumike nguvu kubwa katika kujenga nyumba za walimu ili waweze kuwa karibu na shule na kuwarahisishia utendaji wao huku akitumia fursa hiyo kuwataka maafisa elimukufanya uchambuzi wa kina ili kuona nini hasa kinahitajika katika kuhakikisha shule inapandisha ufaulu.