Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:30 am

NEWS: SHULE 10 BORA NA 10 ZAMWISHO MATOKEO DARASA LA SABA

Dar es salaam: Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Jumanene limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu huku matokeo yakionesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 4.96 ikilinganishwa na asilimia 72.76 mwaka 2017.

Akitangaza matokeo hayo leo Octoba 23, 2018 Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani, Dkt Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 733,103 kati ya 943,318 walitunukiwa matokeo na wamefaulu huku watahiniwa 13, 686 sawa na asilimia 1.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo utoro na ugonjwa.

Zifuatazo ni orodha ya Mikoa, Halmashauri, Manispaa na Majiji 10 yaliyofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo

Mikoa bora hii hapa

1. Dar es Salaam 2. Geita 3. Arusha, 4. Kilimanjaro 5. Kagera 6. Mwanza 7. Iringa 8. Mtwara, 9. Katavi 10. Njombe.

Kwa upande mwingine, shule 10 zilizofanya vizuri zaidi katika matokeo hayo ni pamoja na Raskazone (Tanga), Nyamuge (Mwanza), Twibhoki (Mara), Kwema Modern na Rocken Hill (Shinyanga), St Anne Marie (Dar es Salaam), Jkibira, St Akleus Kiwa nuka, St Severine, Rweikiza zote za mkoani (Kagera).

Hakuishia hapo, Katibu wa Baraza la Mitihani amezitaja pia shule 10 zilizofanya vibaya zaidi katika matokeo hayo. Shule hizi na mahali zilipo ni Mangika (Tanga), Mwazizi (Tabora), Isebanda (Simiyu), Malagano (Tabora), Magana (Mara), Kododo (Morogoro), Mtindili (Tanga), Lumalu (Ruvuma), Chidete (Dodoma), Mavului (Tanga).