Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:47 am

NEWS : SHUGHURI ZA BUNGE KUENDELEA LEBANON LICHA YA KUJIUZULU KWA WAZIRI MKUU

Bunge: Shughuli za serikali ya Lebanon zitaendelea licha ya kujiuzulu Hariri

Bunge: Shughuli za serikali ya Lebanon zitaendelea licha ya kujiuzulu Hariri

Spika wa Bunge la Lebanon amesema shughuli za Baraza la Mawaziri la nchi hiyo zitaendelea kama kawaida licha ya kujiuzulu Waziri Mkuu, Saad Hariri.

Kwa mujibu wa duru za habari zilizo karibu na Nabih Berri, utendakazi wa serikali ya nchi hiyo hautaathiriwa na tangazo la kujiuzulu Hariri akiwa nje ya nchi.

Saad Hariri alijiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu wa Lebanon Jumamosi iliyopita akiwa mjini Riyadh, nchini Saudi Arabia; ambapo pia alitoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Hariri na Mfalme Salman Bin Abdul Aziz wa Saudia mjini Riyadh

Viongozi na wanasiasa mbalimbali nchini Lebanon akiwemo Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah na Adnan Mansour, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo wamesisitizaa kwamba, kujiuzulu Hariri huko Saudia kulifanyika kwa mashinikizo ya utawala wa Aal-Saud hasa kwa kuzingatia kuwa, ushindi wa muqawama nchini Iraq na Syria umezikasirisha mno Marekani, Israel na baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati.

Kadhalika Michel Aoun, Rais wa Lebanon amesema angali anasubiri Hariri arejee nchini ili akibidhi rasmi barua yake ya kujiuzulu kwa mujibu wa taratibu za kisheria, sambamba na kutoa tangazo hilo akiwa ndani ya nchi yake na kwa khiari.