Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:24 pm

NEWS: SHUGHULI ZA SEREKALI YA MAREKANI ZAFUNGWA

Maeneo fulani ya shughuli za serikali ya Marekani zitaendelea kusitishwa kwa siku tano mfululizo, baada ya wajumbe wa baraza la Seneti kushindwa kupiga kura siku ya Jumamosi kutokana na mkwamo kwenye ufadhili wa ujenzi wa ukuta.

Kutokana na kusitishwa kwa shughuli za serikali, ambako kumeshuhudia baadhi ya mashirika yakisitisha operesheni zake siku ya Jumamosi (Disemba 22), Rais Donald Trump amesema atasalia mjini Washington katika sikukuu za Krismasi badala ya kwenda Florida.

Aliandika kupitia Twitter, "Niko Ikulu nikifanya kazi kwa juhudi. Tunaendelea kujadiliana na Democrats juu ya usalama wa mpaka unaohitajika (magenge, madawa ya kulevya, biashara haramu ya usafirishaji binadamu na mengine mengi), lakini tunaweza kutumia muda mrefu".

Trump ameendelea kushinikiza juu ya mahitaji yake ya Dola bilioni 5 kuujenga ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico. Wademocrats wanapinga hilo, na kukosekana kwa mpango thabiti kunamaanisha fedha za shirikisho kwa ajili ya mashirika kadhaa zilikuwa zinaisha muda wake usiku wa Ijumaa.

Mabunge ya Baraza la wawakilishi na Seneti yalifanya vikao vyake siku ya Jumamosi, lakini pande zote ziliahirisha bila ya kufikia makubaliano, na hakuna kura iliyotarajiwa hadi Desemba 27.