Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 1:54 am

NEWS : SHIRIKA LA WAKIMBIZI DUNIANI KUIMARISHA SHUGHULI ZAKE KUSINI MWA NIGERIA

UNHCR kuimarisha shughuli zake kusini mwa NigeriaUNHCR kuimarisha shughuli zake kusini mwa Nigeria

Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR ametangaza kuwa, shirika hilo limeazimia kuimarisha shughuli zake kusini mwa nchi ya Nigeria ya Magharibi mwa Afrika.

Filippo Grandi amesema kuwa, hatua hiyo inachukuliwa kwa shabaha ya kuwasaidia maelfu ya wakimbizi waliokimbia makazi yao kutokana na machafuko huko Cameroon na kwenda katika maeneo ya kusini mwa Nigeria.

Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UUNHCR amebainisha kwamba, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuongezeka wimbi la wakkimbizi katika maeneo hayo ambao wamekuwa wakimiminika kila siku wakitokea nchini Cameroon.

Ghasia za Cameroon

Taarifa ya UNHCR imeeleza kwamba, wafanyakazi zaidi wa shirika hilo la kimataifa la kuhudumia wakimbizi watatumwa katika maeneo hayo ya kusini mwa Nigeria.

Maeneo yanayozungumza lugha ya Kiingereza nchini Cameroon yalitumbukia katika mgogoro wa kijamii na kisiasa sambamba na kuongezeka maandamano tangu mwezi Novemba mwaka jana baada ya wakazi maeneo hayo kudhihirisha azma yao ya kutaka kujitenga.

Raia hao wanaounda asilimia 20 ya watu wote milioni 20 wa Cameroon, wanaamini kuwa, wametengwa na serikali kuu ya nchi hiyo.

Hivi karibuni serikali ya Cameroon ililaani ghasia na machafuko yaliyozuka katika maeneo ya wakazi wanaozungumza lugha ya Kiingereza nchini humo na kutishia kukabiliana na raia hao wanaotaka kujitenga maeneo hayo.