Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:36 am

NEWS: SHIRIKA LA LEAD FOUNDATION LASHUSHA NEEMA MKOANI DOM.

MPWPWA DOM: Shirika la Lead Foundation linayojihusisha na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira kwakufufua visiki hai limesema hadi ifikapo mwaka 2022 litahakikisha linafikia asilimia 50 ya kaya za Dodoma na wilaya zake sabakwa lengo la kukomboa ardhi iliyochakaa ya mashamba na malisho ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa uzinduzi wa mradi huo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkurugenzi wa Shirika la Lead Foundation Njamasi Chiwanga amesema kuwa lengo la Mradi wa Kisiki hai ni kuhakikisha wanafikia Jumla ya kaya laki moja na 80 ambazo zipo katika hali mbaya ya mazingira pamoja na kustawisha miti milioni 14.

Mbali na hayo Njamasi amesema mikakati waliyonayo katika mradi huo ni kuhakikisha wananchi katika kila kijiji kupitia mikutano,makongamano na njia nyingine ikiwemo filamu ya kisiki hai ili kuweza kushirikiana katika kufanikisha kukomboa mazigira na wanatarajia kufikia tarafa mbili katika kila wilaya ili kufikia nusu ya kaya zote za Mkoa huo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri amesema anaunga mkono mradi huo na atahakikisha unafanikiwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbalimbali watakayo hitaji katika kufanikisha mradi huo.



Kwa upande wao baadhi ya wadau waliofika katika uzinduzi wa mradi huo akiwemo Diwani wa kata ya Mlembule Willisoni Mgunga na Shekhe wa Wilaya hiyo Selemani Mohamed wamesema kuwa mpango wa kisiki hai ni mzuri na wana hakika iwapo wananchi wataupokea vizuri baada ya muda mfupi changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya hiyo itakuwa ni historia.

Kisiki hai ni mradi wa miaka mitatu na unatarajiwa kufikia wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ulianza na Wilaya ya kongwa na Sasa ni Wilaya ya Mpwapwa ambapo ulianza na tarafa ya Kongwa na mlali katika wilaya ya kongwa