Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:38 am

NEWS: SHERIA YA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII PSSSF KUANZA KUTUMIKA AUGOST MOSI

DOM: Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,kazi,vijana na walemavu Jenister Mhagama ametangaza tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii PSSSF mara baada ya sheria ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii kupitishwa na Bunge Tarehe 8 February 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma waziri Mhagama amesema serikali imekamilisha maandalizi yote muhimu ya utekelezaji wa sheria ya PSSSF na imeridhika kwamba mfuko hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma utakuwa ni PSSSF na utaanza kutekeleza majukumu yake 1 Augost 2018

Aidha Mhagama amesema hatua hii inamaanisha kuwa wanachama wote ikiwa na wastaafu na warithi waliopo katika mfuko huo iliyounganishwa watahamishiswa katika mfuko huo.

Nao baadhi ya viongozi walioteuliwa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa kazi katika mifuko hiyo wamesema kuwa watahakikisha wanafanya kazi vyema ili kukidhi mahitaji ya mfuko huo kwa watumishi wote

Mbali na hayo waziri mhagama amesema kuwa mifuko hiyo itakuwa chini ya wizara husika huku mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya ya hifadhi ya jamii SSRA ikikihusika kushughulika na mifungo mingine iliyobaki ikiwa ni pamoja na mifuko ya bima ya afya.