Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:37 pm

NEWS: SHERIA YA KULINDA TAARIFA BINAFSI YAJA

DODOMA: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCCRA) inakusudia kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi.

Akifungua kikao cha wadau mbalimbali cha kujadili Mapendekezo ya kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi 2018,Katibu wa Mamlaka ya Mawasailino Tanzania,Dk. Mhandisi Maria Sasabo, amesema kuwa sheria ya kulinda taarifa binafsi itamwezesha mtumiaji wa taarifa hizo kuwa salama na kupatiwa huduma stahiki kulingana na taarifa zake.

Dk.Mhandisi Sasabo amesema kuwa licha ya kuwepo kwa maendeleo ya kidigitali lakini bado hali hiyo imekuwa ikisababisha hasara mbalimbali kutokana na kusambaa kwa taarifa binafsi za mtu husika bila hata ridhaa yake.

“Mnajua kabisa kuwa kwa sasa teknologia imeongezeka kutokana na teknologia hiyo kukua kunaweza kuwepo kwa matumizi halisi na yasiyo kuwa halisi, unaweza kuona picha ya mtu ikitengenezwa na kuonesha uhalisia wa mtu mwingine kumbe siyo yeye.

“Au unaweza kuwa hapa lakini ukaoneka kama uko kwenye mkutano Mwanza na kuonesha mazingira ya mkutano unavyoendelea jambo ambalo siyo kweli hivyo kutokana na hali hiyo ndiyo maana tukaona kuwa ni vyema sasa kukaa na wadau ili kujadiliana na kukusanya maoni ya kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi” amesema Dk.Mhandisi Sasabo.

Amesema kwa kutokuwepo kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi kunaweza kusababisha madhara pamoja na kuwepo kwa madhara mbalimbali yakiwemo ya wizi wa kimtandao pamoja na usambazaji wa taarifa ambazo siyo sahihi kwa mtu binafsi.

Mbali na hilo alisema sheria hiyo itatoa nafasi ya kuwepo taarifa ambazo zinaweza kumlinda mtu binafsi kwa kupatatikana kwa taarifa ambazo hazikinzani, na kila sekta itakuwa ikijitegemea katika utoaji na upatikanaji wa taarifa kama ilivyo sasa.

“Mfano kama mtu atakuwa ni mgojwa taarifa za mgonjwa zitapatikana bila kuingiliwa na mtu mwingine na, taarifa za kifedha nazo zitapatikana kwa taarifa za kifedha na hali hiyo itapunguza tatizo la mtu mmoja kuwa na taariza zinazokinzana” ameeleza.

Hata hivyo amesema kuwa utungwaji wa sheria ya kulinda taarifa binafsi,itazingatia huduma ya taasisi na mtu binafsi pamoja na kujikita kwenye kusudi, usahihi wa taarifa zinazotolewa.

Katika kikao hicho pia wadau wamependekeza kuwepo kwa Idara ya Chombo huru cha kutambua wakusanyaji na wachakataji wa taarifa, ili kuthibiti usafirishaji wa taarifa binafsi pamoja na kulinda maaadili.